Ndorobo
ni wadudu warukao ambao husambaza trypanosomes wasababishao magonjwa ya
trypanosomiasis na nagana kwa mifugo na malale kwa binadamu. Kwa
Tanzania trypanosomiasis ni kati ya magonjwa yanayoathiri binadamu na
mifugo. Ndorobo wana madhara mengi sana kwa mifugo kama vile kuongezeka
kwa vifo, mimba kutoka, kushuka kwa uwezo wa kuzaliana, ukuaji hafifu,
uzalishaji hafifu wa nyama na maziwa, kuzuia matumizi ya
machunga,kuongeza gharama za kuzuia ndorobo n.k. Kwa Afrika inakadiriwa
kuwa ni kilomita za mraba milioni 10 zenye ndorobo ambapo kati ya hizo
ni takribani kilomita za mraba milioni 7 zinazostahili kwa kulishia
mifugo na eneo lililobaki likiwa ni misitu.
Ni 40% ya eneo la Tazania lililoathiriwa na ndorobo ambalolingefaa kwa
shughuli za kilimo na kuchungia mifugo. Aidha anasema ni takribani
mifugo milioni 4.4 na watu milioni4 ambao wako kwenye nafasi kubwa ya
kuambukizwa ugonjwa unaotokana na ndorobo. Inakadiriwa kuwa ni takribani
US$ 7.98 milioni zinapotea kila mwaka kutokana na madhara yatokanayo na
ndorobo (Malele,2011). Kwa kiasi hiki cha pesa inatoa nafasi kubwa
kutafakari ni kwa jinsi gani taifa na wafugaji wanapoteza mapato kama tu
ndorobo wangedhibitiwa.
Tanzania inakadiriwa kuwa na spishi(species) kumi (10) za ndorobo ambazo
zimetapakaa kulingana na uwezo wa kila spishi kustahimili eneo husika.
Aidha inaelezwa kuwa, kubadilika kwa matumizi ya ardhi, ongezekola watu
na shughulu zinazohusu binadamu ni kati ya vyanzo vya kusambaa kwa
ndorobo hapa nchini.
NJIA ZA KUDHIBITI NDOROBO
. 1. Kuondoa vichaka. Hii ni njia iliyoanza kutumika tangu enzi za ukoloni. Ilihusisha kuondoa aidha vichaka vyote au sehemu tu ya vichaka iliyoonesha kuwa kivutio ama makazi ya ndorobo. Kwa upande wa mazingira si rafiki sababu husababisha eneo kuwa wazi hivo kuwa na madhara mengi. Hivo haitumiki sana ijapokuwa inaweza kutumika kwa kuzingatia usalama wa mazingira. 2.2. Kutumia kemikali
Hii ni njia ya kutumia dawa ya kuulia wadudu ambapo inaweza kupuliziwa kutoka angani(aerial spraying) kwa kutumia vifaa maalumu ama kupuliziwa kutokea ardhini(ground spraying), kila njia ina madhara yake na faida zake na viumbe vingine pia huweza kuathirika kutokana na kemikali inayotumika kuua ndorobo.Kemikali zinazoweza kutumika ni Dieldrin (a residual organochloride), Endosulfan (Thiodan; a non-residual organochloride) na Synthetic pyrethroids. 3. Sterile male release technique
Hii ni njia inayotumika kwa kuandaa madume ya ndorobo ndani ya maabara.Madume haya huondolewa uwezo wa mbegu zake kutungisha halafu huachiliwa kwenye eneo liliothiriwa na ndorobo. Ni njia ya gharama sana. Ijapokuwa kutokana na (Bonomi et al., 2011),G. fuscipes ina onekana kuwa tofauti katika njia hii. Njia hufanya ufanisi zaidi kama eneo linalokusudiwa ni dogo pia idadi ya madume yaliyo ondolewa uwezo wa kutungisha maabara yanatakiwa kuwa na idadi kubwa kuliko madume yaliyoko eneo husika. 4. Kutumia mitego
Hutengenezwa kwa kutumia kitambaa cheusi na bluu. Rangi nyeusi huwavuta ndorobo na kutua kwenye rangi nyeusi hivyo kuweza kuvutwa kwenye kifaa cha kukusanyia au sehemu ilikopakwa kemikali ya kuua ndorobo. Lakini pia kemikali za kuwavutia kama acetone, mkojo wa ngombe au mbogo huweza kutumika sababu hutoa harufu ya kuwavuta. Kuzingatia, kuna mitego ya aina nyingi kulingana na aina(spishi) ya ndorobo.Hizo ni baadhi ya njia za kudhibiti ndorobo ambazo hutumika katika maeneo yaliyo athirika na ndorobo.

No comments:
Post a Comment