Gwatamala |
Kwa kiingereza huitwa Guatemala grass.
Na kiswahili chake hujulikana kama nyasi aina ya Gwatemala.
Asili yake ni kutoka nchini Mexico. Ni nyasi ambazo hudumu kwa muda
mrefu(perennial), Huota na kukua kwa kusimama(erect) kwa urefu wa mita
2-3.
Huchomoza matawi kutoka kwenye vinundu(nodes) vya juu.
Hupandwa kwa kutumia vishina katika kipindi cha mwanzo wa msimu wa mvua.
Mfano wa vishina , kushoto ndiyo mfano wa kishina kilichoandaliwa kupandwa. |
Hupandwa ndani ya mashimo ambayo yanakuwa umbali wa sentimita 50-65 kati ya shimo na shimo ili kutoa nafasi ya kutosha baina ya nyasi. Hupandwa katika mistari na kati ya mstari mmoja na mwingine iwe ni mita 100.
Mfano wa jinsi ya kupanda vishina vya gwatamala.
|
Mfugaji anaweza kuandaa shamba na kupanda nyasi za gwatamala kwa ajili
ya mifugo. Mahitaji ya kilimo hiki ni kwenye udongo wenye rutuba, Gwatamala huitaji 400 kg nitrogen, 80 kg phosphorus, 50 kg
potassium, 50 kg calcium na 50 kg za magnesium kwa mwaka kwa hekta (Risopoulos, 1966).
Ijapokuwa nyasi hizi hupendelea sehemu zenye mvua ya kutosha lakini pia
huweza kukua vizuri katika maeneo yenye udongo mzuri yanayopokea mvua
kwa wastani wa 600mm kwa mwaka. Na wakati wa kiangazi hupunguza uwezo wa
kuzalisha malisho. Hustahimili ardhi yenye asidi na aluminium lakini
nyasi hizi hazistahimili maeneo yenye tatizo la kukumbwa na mafuriko.
Nyasi huweza kuwa tayari kuvunwa miezi sita baada ya kupandwa lakini
huchukua tofauti ya miezi minne tu kuvunwa msimu kwa msimu.
Ni nyasi nzuri kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa kwa kukata na kulisha
(green chop-chop for
zero grazing) lakini pia nyasi za gwatamala zinaweza kutunzwa kwa mfumo
sileji kwa ajili ya matumizi ya baadae katika msimu wa kiangazi.
No comments:
Post a Comment