Wednesday, 4 October 2017

MABUA YA MAHINDI NI CHANZO KIZURI CHA CHAKULA KWA MIFUGO.

Huko nchini India baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitumia mabaki ya mahindi (mabua) kuboresha uzalishaji wa ng'ombe wa maziwa. Walikiri kuona mabadiliko chanya kutokana na ulishaji wa mabua mifugo yao. Maandalizi ya mabua kwa ajili ya mifugo yalikuwa kamaifuatavyo;


  • Mabua yanakatwa kutoka shambani
  • Kisha hukatwa katwa kwa mashine/panga kupata vipande vidogo vidogo ili kuongeza kiwango cha mifugo kula chakula kingi (feed intake)
  • Mabua yaliyokatwa katwa hulowekwa kwa masaa 3-4 ndani ya maji
  • Kisha hutolewa kwenye maji na kuchanganywa na chumvi chumvi + madini muhimu
  • Kisha ng'ombe hupewa kama chakula
Hata hivyo changamoto kubwa ya mabua ni ukosefu wa viini lishe vya kutosha, protini kwa ajili ya mifugo. Pia wingi wa nyuzi nyuzi ngumu (lignin content) hupunguza kiwango cha kuliwa. Hata hivyo nyuzi nyuzi ngumu hupunguzwa kwa kukatwa katwa katika vipande vidogo vidogo. Hivyo mfugaji hutakiwa kuwa na vyakula vingine kwa ajili ya kuboresha kiwango cha viini lishe kwenye chakula cha mifugo/n'gombe. Jaribu kuboresha ufugaji kwa kuboresha mabaki ya mahindi uone maajabu yake.

Kwa ushauri zaidi kuhusu malisho tuandikie ujumbe au wasiliana nasi kwa
Barua pepe wataalamumalisho@gmail.com

No comments:

Post a Comment