Na,
FLOIDIN JOHN LINUS
floidinjohn@gmail.com
ARDHI ILIYOATHIRIWA NA SHUGHULI ZA UFUGAJI |
Hapa lazima tuoneshe utofauti wa mtaalamu wa usimamizi na
uendelezaji wa nyanda za malisho na wataalamu wengine.
Ni kweli ndani ya nchi yetu tunakabiriwa na maeneo yenye
kuathiriwa na mikusanyiko ya mifugo eneo moja na kusababisha uharibifu wa
mazingira na migogoro. Mikusanyiko hii chanzo chake ni katika hatua za
utafutaji wa malisho, maji, kukimbia magonjwa ya mifugo na sababu zingine za
kijamii.
Mikusanyiko hii imeathiri ardhi na kusababisha mmomonyoko wa ardhi na
makorongo, uharibifu wa vyanzo vya maji, migogoro ya mara kwa mara na uharibifu
wa malisho.
Hata hivyo mikusanyiko hii imeonekana kuzidi kuongezeka
kadri siku zinavyokwenda maana yake ni kwamba wafugaji wetu wanakumbana na
changamoto nyingi machungani.
Ukisikiliza majadiliano ya watu wengi wanasema kuwa wafugaji
wanatakiwa kutambua kuwa sasa ardhi imekuwa na matumizi mengi lazima wajifunze
kutulia sehemu moja na kuzalisha kitaalamu na kisasa zaidi. Ni kweli lakini
mabadiliko haya yanapofanyika wahusika wakuu hawaangalii mbadala wa wafugaji
waliokuwa wanatumia maeneo haya, hatimaye hutoa nafasi ya wafugaji
kutangatanga.
Mfugaji anakabiliwa na marekebisho ya matumizi ya ardhi
yasiyojali mazingira rafiki ya shughuli yake.
Ufugaji unaonekana kama shughuli inayostahili kufanyiwa
kwenye maeneo yasiyofaa kwa kilimo(remote & unproductive areas), lakini
binafsi hii hoja huwa naipinga kwa sababu kuu mbili,
1)Tukisema ufugaji ufanyike katika maeneo yasiyofaa kwa
kilimo, swali ni Je,katika karne hii yenye teknolojia za juu sana ni eneo gani
lisilofaa kwa kilimo?. Mfano, teknolojia za umwagiliaji,mbegu bora za nafaka na
mbolea.
2) Mahitaji ya malisho ni sawa kabisa na mazao ya nafaka,
mfano mbolea ya kutosha na maji, vyote hivi hutimiza mahitaji ya mwili wa
mnyama ili kufikia uzalishaji wenye tija zaidi na bora kwa mtumiaji.
Kwa kiwango kikubwa misongamano au mikusanyiko hii
inasababishwa na watumiaji wengine wa ardhi wasiotoa mbadala wa mfugaji kupata
mahitaji yake.
Mfano,
ü
Kumzuia mfugaji kuharibu vyanzo vya maji ni
vizuri sana, lakini kumzuia mfugaji pasipo kumtengenezea njia mbadala ya
kunyweshea mifugo yake pasipo kuathiri vyanzo vya maji ni mbaya zaidi.
ü
Kumwondosha mfugaji katika ardhi yenye rutuba
ili kupanua shughuli za kilimo ni vema lakini kumwondosha bila kumwandalia
sehemu nyingine yenye mahitaji stahiki ni kumwonea.
ü
Kumwondoa mfugaji ili apishe uwekezaji ni vema
kwa uchumi wa nchi, lakini hatari ni pale asipoandaliwa eneo zuri la
kuhamishiwa.
ü
Upanuzi wa maeneo tengefu(reserves) kwa ajili ya
mapori na wanyama pori ni vizuri lakini unapomuondosha eneo husika
unamtengenezea mbadala gani?
ü
Kukabidhi mamlaka ya vijiji kutenga maeneo ya
malisho, ni vizuri lakini watu hawa wana elimu ya mifugo na wanajua ni maeneo
gani na yenye sifa gani yanafaa kwa ajili ya mifugo?
Hiyo yote ni baadhi ya mifano
inayosababisha mikusanyiko mikubwa ya mifugo kutokana na kukimbia sehemu
mbalimbali zenye changamoto. Hivo ni ukweli kwamba kwa asilimia kubwa
misongamano hii inasababishwa na watumiaji wengine wa ardhi japo mfugaji ndiye
anaonekana tatizo.
KUPUNGUZA WINGI WA MIFUGO ENEO MOJA BILA KUUZA MIFUGO.
Hapa ndipo mtaalamu wa malisho
anaweza kutofautiana na maamuzi ya wataalamu wasio wa machunga wasiojua sifa za
mifugo kwenye machunga(grazing behavior).
Ø
Miundombinu ya maji, hii inaweza kuwa suluhisho
la misongamano na kupunguza mikusanyiko ya mifugo kwenye machunga pasipo kuuza
mifugo. Kupangilia umbali wa vituo vya maji(water sources) kulingana na aina ya
mifugo iliyopo ndani ya machunga.Hii itasaidia kupunguza msongamano.
Ø
Kubadilisha maeneo ya kuchungia kufatana na
umri, breed na spishi(species). Mfano, ndama wanaweza kuchungiwa maeneo yenye makorongo,
mteremko mkali (rough terrain) hii pia itapunguza msongamano.
Ø
Kuwa na spishi tofauti ya mifugo hii itasaidia
mifugo ya spishi tofauti kuweza kutumia aina tofauti ya aina ya mimea na maeneo
tofauti.
Ø
Kagua eneo la machunga yawezekana msongamano wa
malisho unasababishwa na uvamizi wa vichaka, mimea vamizi, magonjwa au wadudu
hatarishi kama ndorobo n.k.
Utaalamu wowote ndani ya machunga ni vyema ukatizama
kuongezea ardhi uwezo wa kuhudumia mifugo mingi zaidi ili kustawisha ufugaji
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment