Mifugo kutanga tanga kutoka eneo moja hadi jingine limekuwa ni jambo la kawaida hapa nchini. Haswa kutokana na sababu mbalimbali kama mpangilio mbovu wa matumizi ya ardhi, kiangazi, magonjwa, shughuli nyingine za kiuchumi n.k. Hali hii imewafanya wafugaji kuhama hama wakitafuta maeneo mapya yenye malisho na maji ya kutosha. Hata hivyo mfumo huu si salama kabisa katika mazingira na uhakika wa ongezeko la kipato. Ni wakati muafaka wa kuhakikisha mfugaji unakuwa na uwezo wa kuzalisha malisho ya kutosha katika eneo lako ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wako.
Wasiliana nasi tukupatie mbinu na ushauri namna bora ya kuzalisha malisho na kuepukana na kuhama hama kila mara.
Wasiliana nasi kwa kuacha ujumbe au barua pepe, wataalamumalisho@gmail.com
Nahitaji kujifunza njia z kuzalisha nyasi kwaajili y mifugo
ReplyDelete