Tuesday, 3 October 2017

MIMEA INAYOWEZA KUTUPA VIASHIRIO VYA HALI YA MACHUNGA.

Chanzo ni Prof E.J. MTENGETI  

Idara ya sayansi ya mifugo,samaki na malisho
Sokoine University of agriculture.
     
 Ili kutambua hali ya machunga lazima kutambua mimea muhimu yenye kuashiria hali ya machunga. Uwepo au kutokuwepo kwa mimea fulani ndani ya machunga ni kiashiria tosha cha hali ya machunga. Na hii itakupa fursa kutambua kama unatakiwa kuchukua hatua gani madhubutu kurekebisha au kudumisha hali hiyo. Mimea iliyotolewa maelezo (siyo picha) na Prof. E.J. Mtengeti ni kama ifuatavyo:-
Kutambua afya ya machunga
Brachiaria brizantha
 a) Kuna mimea ambayo ukigundua  inapungua sana ndani ya machunga (decreasers) basi ujue malisho yanachungiwa sana. Mimea inayopendelewa sana na mifugo ndiyo hupungua kadri machunga yanavyochungiwa kwa mudamrefu zaidi. mfano mzuri ni Brachiaria brizantha.




Sporobolus pyramidalis.
b)Kuna mimea ambayo huongezeka kadri machunga yanavyozidi kuchungiwa (increasers). Mimea hii siyo yenye kupendelewa na mifugo. Manake ni kwamba mimea inayopendelewa (decreasers) hupungua na mimea mingine(increasers) huibuka. Ukigundua mimea hiyo basi ni kiashiria cha kuzidisha kuchunga katika eneo hilo. Mfano ni Sporobolus pyramidalis.
Mimea hii ni hatari sana, kwa sababu ukiiruhusu iendelee kukua huweza kuathiri mimea mingine ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifugo. Hivyo mimea ya aina hii inatakiwa kudhibitiwa haraka sana mara tu baada ya kuona viashiria vyake.
c) Mimea vamizi (invaders). Mimea yenye sifa za kipengele (a) na (b) inapochungiwa sana na kuliwa
Dactyloctenium aegyptium
Rhynchelytrum repens
basi hupungua ndani ya machunga kisha mimea mipya isiyoliwa
kabisa na mifugo huvamia eneo hilo. Mimea hiyo ni kama vile Dactyloctenium aegyptium na Rhynchelytrum repens. Mimea hii haitakiwi kabisa ndani ya machunga kwa sababu ya madhara yake kama vile, kupunguza chakula cha mifugo, kushambulia mimea muhimu pamoja na uwezo wake mdogo wa kulinda udongo dhidi ya tatizo la mmomonyoko.

Mimea inayoweza kuashiria uwepo wa maji.
Acacia xanthophlea
Sycamore
Kuna mimea ndani ya machunga ambayo ni kiashiria kizuri cha uwepo wa maji karibu kabisa na uso wa dunia. Mimea hii ni muhimu haswa kwa meneja/ mfugaji anayetaka kuchimba kisima kwa ajili ya kupata maji ya mifugo na kumwagilizia malisho yake. Mimea hii ni kama vile, Sycamore, Acacia xanthophlea, Acacia elatior.


Kutambua hali ya udongo.
Kuna mimea ndani ya machunga ambayo hutoa viashiria vya hali ya udongokatika eneo husika. Mfano ni,
Cynodon nlemfuensis
1) Cynodon nlemfuensis hii mimea huashiria uwepo wa wingi nitrojeni katika udongo wa eneo husika na udongo wenye unyevunyevu wa kutosha.

Conyza stricta
2) Conyza stricta  hii mimea pia hupendelea udongo wenye nitrojeni nyingi.
Hivyo ni kiashiria cha nitrojeni nyingi kwenye machunga.
3. Imperata cylindrica huashiria udongo wenye pH ndogo yaani asili ya asidi.




Imperata cylindrica

IMEANDALIWA NA 
Linus, Floidin John

No comments:

Post a Comment