- Cenchrus ciliaris (Buffel grass)
Buffel grass |
chakula cha mifugo. Zina uwezo wa kustahimili ukame kwa muda mrefu hivyo
kupendekezwa kama nyasi zenye kuweza kulimwa maeneo kame hapa nchini
kama Dodoma, Tabora na Singida. Hutoa mizizi yenye kwenda ardhini umbali
wa hadi meta 2, hivyo huweza kufyonza maji ardhini mbali zaidi. Ni
rahisi kupanda na hutoa malisho kwa wingi haswa zikipandwa na mbolea.
Ikivunwa mwanzoni kabisa baada ya kuchomoza maua,huzalisha malisho mengi
na bora ambayo huweza kutunzwa kama hei (hay). Akiba hii huweza
kutumika wakati wa kiangazi kulishia mifugo. Buffel grass hustahimili
moto (FAO, 2010). Haina uwezo wa kustahimili maeneo yenye kukumbwa na
mafuriko (waterlogging area) na huweza kufa kwa baada ya takribani siku
6 (Ecoport, 2010). Huweza kuvumilia kuchungiwa (over grazing) hata
kukanyagwa( trampling.
2. Urochloa mosambicensis
Hizi
ni nyasi zenye kustahimili ukame na kudumu zaidi ya mwaka mmoja
(perennial). Hutofautiana kimo au wastani wa ukuaji pamoja na tabia
(habit) ya ukuaji kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa ya
eneo husika(climate), udongo (edaphic factors) n.k
Huota
katika udongo tofauti ijapokuwa huitaji zaidi udongo wenye mbolea,
kuanzia udongo wenye asili ya ufinyazi (clay soil) na ule wenye asili ya
kichanga (sandy soil). Huweza kustahimili udongo wenye asili ya
u-asidi, alkali na chumvi chumvi.
Hata
hivyo, kwa nchini mwetu wafugaji wetu hawajajikita katika ulimaji wa
nyasi aina hii lakini ni chanzo kizuri cha chakula kwa ajili ya mifugo.
Ni
nyasi ambayo haijathibitika kuwa na sumu yoyote kwa mifugo au kuwa na
uhusiano na magonjwa, hivyo ni chakula kisicho na madhara kwa mifugo3. Eragrostis superba (Masai love grass)
Masai love grass |
Hujiotea kwa asili hapa nchini sababu ya wakulima au wafugaji wengi kutokujikita katika kilimo cha nyasi za kulishia mifugo.
Hukua kwa haraka sana na huwa na hali ya umbijani kwa
takribani mwaka mzima. Huweza kustahimili sehemu zenye udongo wa chumvi
chumvi na alkali. Hustawi zaidi katika maeneo yenye udongo asili ya
kichanga ijapokuwa hata udongo mwingine kama mfinyanzi hustawi. Hata
hivyo ijapokuwa hukua haraka lakini hupoteza ubora(stemmy and
unpalatable) kwa ajili ya mifugo kadri inavyozidi kukomaa pia kiwango
cha virutubisho hushuka sana.
4. Bothriochloa insculpta ( Creeping bluegrass)
Creeping bluegrass |
Hutumika kama nyasi za kuchungia au kutengenezea hei(hay)
katika mashamba ya kufuga ng'ombe wa nyama (hukataliwa na ng'ombe wa maziwa).
Huweza kutumika kwa kuchungia au kukata nyasi na kulishia bandani (cut and carry).
Ni bora zaidi kama hazijakomaa sana sababu ubora wake(palatability) hupungua kadri nyasi zinavyokomaa.
Hustahimili ukame, kuchungiwa(heavy grazing) moto na
mafuriko japo ni kwa kipindi kifupi tu.
Huweza kustawi katika aina tofauti ya udongo japo haistawi vizuri maeneo yenye udongo wa kichanga .
Nyasi hizi hazistawi katika maeneo yenye kivuli au udongo wa asidi.
MALISHO AINA YA MIKUNDE YENYE UWEZO WA KUSTAHIMILI MAENEO YENYE ASILI YA UKAME
1. Stylosanthes humilis
Uwezo wake wa kutengeneza nitrojeni (nitrogen fixtion),
kustahimili ukame, kuboresha hali ya udongo na kuwa chanzo cha protini
kwa mifugo ni kati ya faida za huu mkunde. Mkunde huu una uwezo wa
kutumia(extract) hata madini ya fosiforasi yaliyo kidogo sana kutumika
kwa ajili ya mimea mingine. Huweza kuoteshwa kwa kuchanganywa na baadhi
ya nyasi zisizo zalisha kivuli kama vile Cenchrus ciliaris, Heteropogon contortus na Urochloa mosambicensis. Mkulima
anaweza kuchungia moja kwa moja, kukata na kulishia bandani,
kutengeneza hei au saileji. Hustahimili ukame pamoja na udongo wa
kichanga au tifutifu. Hata hivyo, imethibitika mikunde hii kuwa sumu kwa
baadhi ya kupe wasababishao magonjwa kwa ng'ombe (acaricidal effects)
(Muro Castrejón et al., 2003; Fernandez-Ruvalcaba et al., 1999).
2. Stylosanthes hamata
Hayo ni baadhi ya malisho yawezayo kustahimili ukame na kuwa msaada kwa mfugaji.....
No comments:
Post a Comment