Najua unaelewa vizuri kuhusu papai. Wengine mnayalima au yanajiotea katika mazingira ya nyumbani. Mnayatumia kama matunda kwa ajili ya kuboresha afya za familia kutokana na faida mbalimbali za kiafya.
Lakini papai ni muhimu pia kwa kuku hapo nyumbani. Kwa kutibu maradhi ya kuhara kwa kuku hatutumii matunda tena bali majani yake tu. Ni hivi msomaji, chukua jani la mpapai kisha twanga vizuri upate mfano wa kisamvu kilichotwangwa vizuri. Andaa angalau lita 2.5 za maji safi kisha changanya vizuri na uache kwa muda. Wape kuku wanywe siku nzima maji hayo tu siku nzima. Unaweza kuwapatia wakanywa angalau siku 4 kwa wiki lakini hakikisha kila siku unaandaa dawa mpya. Zingatia kuwapa mchanganyiko huu kabla ya kuona hata dalili za kuharisha.
Kinga ni bora kuliko tiba.
No comments:
Post a Comment